Westham United Chaguo Bora Zaidi kwa Wachezaji wa Ghana
Wachezaji wengi wa kimataifa wa Ghana wamehudumu katika klabu ya Westham United ya England.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana Chris Hughton alicheza katika klabu ya Westham United miaka ya 1990 mpaka 1992.
John Paintsil alijiunga na klabu ya Westham United baada ya komba la Dunia la mwaka 2006 na jina lake lilipendekezwa na Yossi Benayoun kwa kocha wao wa kipindi hicho Alan Pardew.
Baada ya kusajiliwa John Paintsil alihudumu kwa wagonga nyumyo wa London Westham United kuanzia 2006-2008.
Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew alijiunga na Westham United mwaka 2016 na alivunja rekodi ya usajoli wa klabu hiyo
Andre Ayew alijiunga Westham United kw gharama ya £20.5m kutoka katika klabu ya Swansea na huu ndiyo ulikua usajili ghali zaidi kwa mwaka huo ndani ya klabu hiyo.
Andre Ayew alihudumu katika klabu ya Westham United kuanzia mwaka 2016 mpaka 2018.
Wachezaji hao pia walihudumu katika kipindi cha misimu miwili.
#