Kocha Enzo Maresca alithibitisha uamuzi huo kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Brighton, akieleza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atapumzishwa hadi baada ya mapumziko ya kimataifa ya Oktoba.

“Tumeamua kumlinda Cole kidogo, ili hali yake isitindike zaidi. Tumefanya uamuzi wa kumpumzisha kwa wiki mbili au tatu, hadi mapumziko ya kimataifa, kuona kama baada ya muda huo anaweza kupona kwa asilimia 100,” alisema Maresca.




Palmer alilazimika kutoka uwanjani kipindi cha kwanza katika kichapo cha 2-1 dhidi ya Manchester United wiki iliyopita. Tatizo hilo lilianza kujitokeza wakati wa maandalizi mafupi ya msimu baada ya Chelsea kutwaa Kombe la Dunia la Klabu mwezi Julai, na hadi sasa ameanza michezo mitatu pekee kati ya saba msimu huu.

Maresca alifafanua kuwa upasuaji hauhitajiki, lakini jambo la msingi ni kudhibiti maumivu hayo ipasavyo:

“Sidhani kama anahitaji upasuaji; ni suala la kudhibiti maumivu ya nyonga yake tu.”

Kocha huyo pia aliwataka mashabiki wawe na utulivu, akisisitiza kuwa Chelsea itajipanga bila Palmer

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement