Gwiji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney amemtaka mshambuliaji Marcus Rashford kuachana na klabu hiyo katika dirisha la usajili la kiangazi na kutafuta changamoto mpya kwingine.

Rashford ameonekana kupata wakati mgumu msimu huu kutokana na ubutu wa kufumania nyavu ambao amekuwa akiuonyesha ambapo hadi sasa amefunga mabao nane tu katika mechi 38 za mashindano tofauti alizoichezea timu hiyo.

Ni tofauti na msimu uliopita ambapo alipachika mabao 30 katika mashindano tofauti jambo ambalo limemuibua Rooney ambaye amesema kuwa kama Rashford ataendelea kubakia Man United ataweka rehani kipaji chake.

Rooney anaamini kuwa kinachomuangusha Rashford ndani ya Man United hivi sasa ni kupoteza hali ya kujiamini hivyo ili aepukane nacho anapaswa kutafuta malisho mengine nje ya klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka nane.

"Amekuwa na msimu mgumu. Wote tunajua kwamba amepewa uwezo na ana sifa zote za kumuwezesha kuwa mchezaji wa daraja kubwa duniani.

"Hiki ndio kitu kinachochanganya. Msimu uliopita alifunga idadi kubwa ya mabao. Lakini msimu huu hajaendelea. Haonekani na furaha akiwa anacheza," alisema Rooney.

Rooney alisema hakuna sababu kwa Rashford kuendelea kung'ang'ania kuitumikia Man United wakati mambo yanazidi kumuendea vibaya hivyo anapaswa kujiamulia mwenyewe.

"Unashangaa uamuzi wake bora ni kutoka nje ya klabu na kuanza upya? Lakini yeye ni mtoto wa Manchester. Nitafurahi kumuona akirudi katika ubora wake, kufunga na kusaidia klabu kushinda mataji. Lakini kwa namna fulani amekuwa na msimu mgumu," alisema Rooney.

Rashford hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka Manchester United haid 2027 akiwa analipwa kiasi cha Pauni 300,000 kwa wiki.

Hivi karibuni alikanusha taarifa za yeye kutaka kuondoka ingawa PSG imekuwa ikitajwa kuwa inamnyemelea nyota huyo ili kuziba pengo la Kylia


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement