Beki wa Manchester United Raphael Varane anaweza kurejea Real Madrid Januari hii.

Hii ni baaada ya beki wa kati David Alaba kupata majeraha yatakayo muweka nje msimu huu, huku Eder Militao akiwa majeruhi pia.

Kulingana na mwandishi wa habari wa BILD Christian Falk, Real sasa wanataka kumrejesha Varane Bernabeu.

Hakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza msimu huu na tayari kulikuwa na uvumi kwamba anaweza kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement