Jean Florent Ibenge Kocha wa zamani wa Leopards timu ya Taifa ya DRC, anawindwa na Mali kuchukua nafasi ya Éric Chelle ambaye amefukuzwa kazi kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Ibenge Kocha wa zamani wa AS Vita Club ya Kinshasa na RS Berkane ya Morocco kwa sasa akiwa katika klabu ya Al Hilal SC ya Sudan, amewekwa kwenye rada za Shirikisho soka la Mali ili kuchukua nafasi ya kocha aliyefutwa kazi Eric Chelle.

Kwa sasa akiwa nchini Tanzania na timu yake ya Al Hilal SC ambayo alifanikiwa kuifikisha kwa misimu miwili mfululizo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kukosekana kwa bingwa nchini Sudan kufuatia vita ya wenyewe kwa wenyewe, fundi huyo wa soka anasikiliza ofa kutoka kwa timu hiyo ya Taifa ya Mali.

Bado Ibenge ana mkataba na Al Hilal ambao ili kumng’oa mkataba itabidi kulipa hela ya kuuvunja mkataba huo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement