Klabu ya Simba imeripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na aliyewahi kuwa kocha wa Mamelodi Sundowns, Steve Komphela ambaye hivi sasa yupo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Abdelhak Benchikha kama kocha mkuu wa kudumu klabuni hapo.

Simba Sc ambayo imekuwa chini ya Mtanzania Juma Mgunda kwa muda inatafuta kocha mpya kwa ajili ya kampeni za msimu ujao.

Aidha zipo ripoti kuwa Juma Mgunda ameruhusiwa kuondoka klabuni hapo kwa ajili ya kwenda kukinoa kikosi cha Coastal Union.

Inadaiwa kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma hana sifa za kuiongoza Coastal kwenye michuano ya kombe la Shirikisho hivyo Mgunda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kampeni za michuano hiyo msimu ujao.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement