SIMON MSUVA ATAMBULISHWA AL NAJMAH YA SAUDI ARABIA
Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Tanzania, Simon Msuva ndio basi tena Yanga. Hii ni baada ya kutambulishwa Al Najmah inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Saudi Arabia.
Kipindi cha dirisha dogo la usajilikulikuwa na tetesi za nyota huyo aliyewahi kutamba akiwa na Yanga, huenda akarejea kwenye timu hiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara akiwa mchezaji huru baada ya kuvunjiwa mkataba na JS Kabylie ya Algeria.
Wakati wengi wakiamini anarudi Jangwani alikoondoka tangu msimu wa 2017/18 na kutua Difaa El Jadida, msuva hakurejea kucheza Ligi Kuu Bara na ameendelea kucheza nje ya nchi ikiwani mara ya pili anarudi Saudi Arabia kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
Baada ya utambulisho huo, kwenye akaunti ya klabu ya Instagram, Msuva aliongea akifurahia kujiunga na tỉmu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi hiyo, iko nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 18 na ina pointi 25.
"Nafurahia kusaini Al Najma, nafurahi kurudi Saudi Arabia na tutaonana baadaye" alisema Msuva.
Msuva atajiunga na timu hiyo baada yakumaliza mechi za Stars ambayoinacheza leo na DR Congo mchezo wamwisho wa hatua ya makundi kwenye Fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast.
Hii ni timu ya tano kwake kucheza nje ya nchi tangu alivyoondoka Yanga msimu wa 2017-18 na amepita Difaa El Jadida na Wydad Casablanca ya Morocco, Al Qadsiah ya Saudi Arabia na JS Kabylie ya Algeria.
Kwenye Fainali za Afcon ameifungia bao moja Stars dhidi ya Zambia nakufikisha mabao 22 tangu aanze kuichezea timu hiyo.