SHIRIKISHO LA FIFA LAIONDOLEA ADHABU YA KUTO KUSAJILI KLABU YA YANGA SC
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea Young Africans adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kukamilisha malipo ya aliyekuwa mchezaji wao Lazarus Kambole.
Awali mchezaji huyo raia wa Zambia alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC kwa kushindwa kumlipa ujira wake.
Kambole alishinda kesi hiyo, na Young Africans ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza uamuzi huo na kusababisha ifungiwe kusajili.
Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Young Africans kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.