Mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.

Mané (31) raia wa Senegal anatarajiwa kuungana na Cristiano Ronaldo klabuni hapo ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu aondoke Liverpool na kujiunga na Mabingwa hao wa Bundesliga.

Mané alijiunga na Bayern Munich msimu uliopita kwa ada ya pauni 34 na kuifungia Bayern Munich magoli 7 tu kwenye mechi 25 huku akijikuta kwenye ugomvi na nyota wa Ujerumani Leroy Sane uliopelekea kupigwa faini.

Mané anatarajiwa kuungana nyota wengine waliotua klabuni hapo kutoka Ulaya wakiwemo Marcelo Brozovic kutoka Inter Milan na Seko Fofana kutoka Lens.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement