Real Madrid wako tayari kujadiliana na Chelsea kuhusu mkataba wa kudumu wa Kepa Arrizabalaga, lakini hawatalipa zaidi ya euro milioni 17.5 kwa kipa huyo Mhispania mwenye umri wa miaka 29 ambaye aliigharimu The Blues takriban euro milioni 71.6 miaka mitano iliyopita.

Kepa alijiunga na Chelsea kutoka Athletic Bilbao kwa £71m Agosti 2018 - ada kubwa zaidi kuwahi kulipwa kwa kipa. Hata hivyo, baadaye alipoteza nafasi yake kwa Edouard Mendy na kuirejesha msimu uliopita wakati kipa huyo wa Senegal alipoumia. Mendy ameondoka Chelsea baada ya kumuuza kwa Al-Ahli ya Saudia mwezi Juni. Kepa, ambaye ameichezea Chelsea mechi 163, pia alikuwa akihusishwa na kuhamia Bayern Munich, ambapo mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Manuel Neuer amepata jeraha. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement