Beki wa Manchester United Raphael Varane ataondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na kikosi cha Old Trafford kutoka Real Madrid msimu wa joto 2021 kwa ada ya awali ya takriban £34m na amecheza mechi 93.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa aliisaidia United kushinda Kombe la Carabao mwaka wa 2023 wakati kikosi cha meneja Erik ten Hag kilipoifunga Newcastle United kwenye fainali.

"Kila mtu United anamshukuru Rapha kwa huduma yake na kumtakia heri kwa siku zijazo,"ilisema taarifa ya United.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement