PSG Wakubali Kumuuza Mchezaji Wao Kylian Mbappe
PSG imekubali kumuuza mshambuliaji wake, Kylian Mbappe (24) kwa ofa ya Pauni milioni 259 [TZS bilioni 811] iliyowekwa mezani na Al Hilal ya Saudi Arabia.
Mbappe na PSG wamekuwa katika mvutano wa kimkataba, klabu ikimtaka aongeze mkataba vinginevyo atauzwa mwaka huu, huku mchezaji akikataa na kusema atasalia hadi mkataba wake utakapoisha mwakani.