Mokwena, ambaye ni mmoja wa makocha vijana wenye rekodi nzuri barani Afrika, anajiunga na timu hiyo baada ya kuachana na miamba ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns ambapo uwepo wa Mokwena kwenye Ligi ya Algeria unaashiria kuibuka kwa vita ya makocha wawili wanaofahamiana vyema na ambao walishawahi kushambuliana kwa maneno nchini Afrika Kusini kwamaana ya Rulani Mokwena na Sead Ramovic.


Ramovic, ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa CR Belouizdad, moja ya timu kubwa na yenye mafanikio nchini Algeria, anatarajiwa kumenyana vikali na Rulani katika kile kinachotajwa kuwa ni “vita ya mafahali wawili.

Mokwena mwenye Umri wa miaka 38 alikaa msimu uliopita katika klabu ya Wydad baada ya kutimuliwa Sundowns, lakini akaachana na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu wa Botola Pro baada ya kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya CAF, hii baada ya kumaliza nafasi ya sita msimu kabla ya kuwasili kwake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement