Mkuu wa Usajili wa Brighton Sam Jewell amekubali kujiunga na Chelsea, Atakuwa sehemu ya mradi wa klabu kuleta na kuchagua wachezaji wapya.

Amewekwa likizo ya majukumu mpaka pale Chelsea watakapolipa fedha ya makubaliano wakati huo Mike Cave na George Holmes watachukua majukumu ya Jewell, klabu Brighton yathibitisha.

Klabu ya Brighton imekuwa sehemu ya kutoa watendaji wao muhimu kwenye klabu nyingine hadi sasa Dan Ashworth alienda Newcastle na Sam Jewell anaenda Chelsea.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement