Kama ilivyo kwa Liverpool kuachana na Kocha wake, Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu huu, ndivyo ilivyo kwa Bayern Munich kuachana na kocha wake Thomas Tuchel ifikapo mwisho mwa msimu huu wa 2023/24.

Kubwa na la kushangaza kuwa vilabu vyote viwili vinamtolea macho Xabi Alonso aliyewahi kucheza vilabu hivyo viwili kwa mafanikio makubwa.

Mkataba wa Alonso na timu yake ya sasa ya Bayer Leverkusen haina masharti ya kumzuia kuondoka ndani ya klabu hiyo hivyo ataruhusiwa kuondoka endapo ataamua mwenyewe.

Ikumbukwe kuwa Alonso ameitumikia Liverpool mwaka 2004 hadi 2009 kisha akatimkia Real Madrid akadumu huko kwa miaka mitano kuanzia 2009 hadi 2014 kisha akaenda kulimalizia soka lake Bayern Munich alikocheza miaka mitatu tangu mwaka 2014 hadi 2017.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement