LIVERP00L ipo kwenye mchakato wakufanya mazungumzo na wawakilishi wa beki wake kutoka England, Trent Alexander-Arnold, 25, ili kumsainisha mkataba mpya wa muda mrefu.

Arnold ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2025, ameahidiwa ofa ya mshahara nusu zaidi ya ule wa Pauni 180,000 kwa wiki anaoupokea kwa sasa.

Alikuwa akitajwa kuwa ni mmoja kati ya mastaa wanaoweza kuondoka Liverpool baada ya kuondoka kwa kocha Jurgen Klopp aliyetangaza kuachana na timu hiyo mwisho wa msimu.

Trent ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Liverpool, amekuwa na msaada mkubwa katika utoaji wa krosi zinazozaa mabao.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 29 za michuano yote akifunga mabao mawili pekee, lakini ametoa asisti 10.

Mbali ya staa huyu Liverpool pia itaingia kwenye mazungumzo nawawakilishi wa straika Mohamed Salah na Virgil van Dijk ambao wote wanahusishwa kuondoka na mikataba yao inakaribia kumalizika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement