MCHEZAJI WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED RUUD VAN NISTELROOY ATEULIWA KUWA KOCHA MSAIDIZI WA KLABU HIYO
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy amejiunga na Mashetani hao Wekundu kama kocha msaidizi chini ya kocha mkuu Eric Ten Hag wote raia wa Uholanzi.
Van Nistelrooy (48) amekubali nafasi ya kuwa kocha msaidizi klabuni hapo licha ya kutakiwa na vilabu kadhaa ikiwemo Burnley kama kocha mkuu wa vilabu hivyo.
Van Nistelrooy aliifungia Man United jumla ya magoli 150 katika mechi 219 katika misimu mitano enzi yake kama mchezaji akishinda taji la Ligi Kuu, Kombe la FA na Kombe la Ligi.
Nistelrooy aliiongoza PSV kutwaa kombe la Uholanzi akiwa kama kocha mnamo 2023 kabla ya kuondoka kabla ya mwisho wa msimu wa 2022/23.