Matajiri kutoka Saudi Arabia bado wanapambana kuhakikisha kipa wa Liverpool, Alisson Becker anatua katika kikosi chao msimu ujao.

Becker amekuwa akitajwa kuondoka Liverpool tangu mwezi uliopita ikielezwa anataka kufanya hivyo ili kupata changamoto mpya na hapo ndipo matajiri hao wa Saudia walipopata fursa ya kuanza kuiwania saini yake.

Taarifa kutoka Teamtalk zinaeleza moja ya sababu zinazomfanya Becker ahitaji ni kuondoka kwa kocha Jurgen Klopp ambaye anaenda kupumzika baada ya kufanya kazi hiyo kwa misimu tisa akiwa Anfield.

Inaelezwa matajiri hao wa Saudia wanataka kumpa kipa huyu mshahara wa zaidi ya Pauni 400,000 kwa wiki kiasi ambacho inaonekana kuwani ngumu kwake kukikataa, licha ya mkataba wake kuwa unamalizika mwaka 2027.

Liverpool ipo tayari kumwachia katika dirisha hili ikiwa itapokea ofa nzuri na inafanya hivyo ili kupata pesa kwa ajili ya kushusha nyota wapya.

Msimu uliomalizika alicheza mechi 32 za michuano yote na kufungwa mabao 32, huku mechi 11 akimaliza bila ya kuruhusu nyavu zake kutikisika.

Liverpool huenda ikahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni ili kumwachia fundi huyu wa kimataifa wa Brazil.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement