Barcelona, Chelsea na Paris Saint-Germain ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Julian Alvarez ambaye ameripotiwa kukataa mkataba wa miaka minne wa kuendelea kusalia Man City.

Hata hivyo, Man City haina mpango wa kumuuza kwa sasa licha ya kupokea maombi ya kwamba anataka kuondoka.

Kwa mujibu wa ripoti timu hizo zipo tayari kulipa Pauni 70 milioni ili kufanikisha mchakato wa kumsajili staa huyu wa kimataifa wa Argentina.

Alverez anataka kujiunga na timu ambayo itampa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza tofauti na ilivyo sasa ambapo licha ya kucheza idadi kubwa ya mechi, nyingi huingia akitokea benchi.

Guardiola bado anatamani kuendelea kusalia na staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2028.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement