MADRID KUWINDA SAINI YA OSIMHEN WA NAPOLI
Real Madrid wanamtaka Victor Osimhen ikiwa hawawezi kumsajili Erling Haaland au Kylian Mbappe.
Kwa mujibu wa Sports, Real Madrid wanaweza kumnunua Osimhen endapo hawataweza kumsajili kati ya walengwa wao wawili wakuu, Mbappe na Haaland.
Watakuwa wanaangalia dili la euro milioni 130 linalozingatiwa na rais Florentino Perez.
Osimhen kwa sasa yuko mbioni kusaini mkataba mpya na Napoli, ambao utamuongezea muda wa kukaa klabuni hapo hadi 2028.
Hata hivyo, mkataba huo mpya unaweza kujumuisha kipengele cha kutolewa cha €130m, ambacho kikosi cha Carlo Ancelotti kitakuwa tayari kuachana nacho kumsajili mchezaji huyo.