Liverpool imeendelea kupambana kwa ajili ya kumsajili straika wa Aston Villa, Ollie Watkins katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo msimu ujao huenda likamkosa Mohamed Salah anayetajwa kuwa kwenye mpango wa kataka kujiunga na Al Ittihad ya Saudi Arabia.

Mabosi wa Liverpool wamevutiwa sana na kuwango cha Watkins alichoonyesha msimu uliopita na alifunga mabao 19.

Kusajiliwa kwa Watkins pia kunatajwa kusababishwa na kitendo cha Barcelona kutaka kumsajili Darwin Nunez.

Kocha mpya wa majogoo hawa wa Jiji la Liverpool, Arne Slot anataka kujenga upya timu na amewaambia wachezaji ambao hawahitaji kubaki kuwa milango ipo wazi.

Hata hivyo, inaonekana kuwa itakuwa ngumu kwa Liverpool kumpata staa huyu kwa bei rahisi kwani ndio mchezaji tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Villa na bado ana mkataba wa zaidi ya misimu mitatu mbele.

Kingine kinatajwa itakuwa ngumu kwa sababu Villa pia itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na hawataki kuuza wachezaji wao muhimu ili wawasaidie kwenye michuano hiyo mikubwa inayoshiriki kwa mara ya kwanza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement