REAL Madrid imeripotiwa itamtambulisha Kylian Mbappe kuwa usajili wa kwanza dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, Jumatatu.

Kikosi hicho cha kocha Carlo Ancelotti, usiku wa Jumamosi kilikuwa na kibarua cha kukabiliana na Borussia Dortmund kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Wembley.

Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la L’Equipe, Real Madrid ilipanga kumtambulisha Mbappe kuwa usajili wa kwanza kwenye dirisha hili saa chache mbele baada ya fainali ya Ulaya.

Taarifa zilidai Mbappe atatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Real Madrid, Jumatatu, huku ikitambua hilo haliwezi kuwa na athari hasi Ufaransa wakati wa fainali za Euro 2024, ambapo mchezo wa kwanza watakipiga Juni 17. Mbappe, amefunga mabao 256 na asisti 108 katika mechi 308 alizochezea PSG.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement