Hizo ni taarifa njema kwa mashabiki wa Aston Villa, ambao wamekuwa wakikoshwa na utendaji kazi wa kocha huyo Mhispaniola, ambaye amewawezesha kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuinoa timu hiyo kwa miezi 19 tu.

Emery alisema: “Nimefurahi sana kwa hatua hii na kuwajibika kuiongoza klabu hii."

Mwenyekiti wa Aston Villa, Nassef Sawiris alisema: “Tunajaribu kutengeneza kitu spesho hapa Aston Villa na Unai ni mtu muhimu kwenye hilo na ndiyo maana amesaini mkataba hadi 2029.

“Wakati tukielekea kwenye historia yetu, sherehe ya miaka 150 kuna mengi ya kuyatarajia wakati Unai akiwa kwenye benchi la ufundi.”

Emery amepewa ruhusu na wamiliki wa klabu hiyo, mabilionea Nassef Sawiris na Wes Edens kuhakikisha anakijenga kikosi na kuwa kwenye makali ya kutisha kwa ajili ya msimu ujao.

Wamiliki hao walikutana na kocha Emery, rais wa klabu kuhusu masuala ya soka, Monchi pamoja na mkurugenzi wa soka, Damian Vidagany kufanya mapitio ya msimu ulivyokuwa.

Sasa kwenye dili hilo jipya, Emery anakuwa kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye historia ya Aston Villa, akiweka kibindoni Pauni 8 milioni kabla ya bonasi, hivyo kiasi hicho ni sawa na mshahara wa Pauni 154,000 kwa wiki.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement