Uongozi wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca, Fadlu David ambaye inaelezwa atatua nchini Ijumaa sambamba na wasaidizi wake.

Kocha huyo ambaye amethibitisha ujio wake Tanzania baada ya kutumia ukurasa wake mtandao wa kijamii ‘Instagram’ kuwaaga viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu aliyokuwa akiifundisha.

“Ulikuwa ni wakati mzuri, msimu mzuri, wachezaji bora, wafanyakazi wenzangu tulikuwa na benchi bora bila kuwasahau mashabiki,” Ni ujumbe wa kocha huyo akiwaaga."

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti kuwa kocha huyo anakuja na wasaidizi wake sambamba na meneja wa timu hiyo.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement