Klabu ya Vitalo FC ya Burundi imeingia mkataba wa mwaka mmoja na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya BS Dynamik, Haruna Ferouz ikiwa ni katika maandalizi ya Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na Ligi Kuu nchini Burundi.

Vitalo FC wawakilishi wa Burundi katika Mashindano hayo ya Kimataifa. 

Miamba hiyo ya Burundi inarejea katika michuano ya Kimataifa baada ya kumaliza muda mrefu bila kushiriki michuano hiyo.

Katika uteuzi huo, aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Sahabo Parris atakuwa kocha msaidizi chini ya kocha Ferouz.

Mbali ya Vitalo FC, Rukinzo FC watakuwa wawakilishi wa Burundi ngazi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement