Klabu ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji Raia wa Ivory Coast Ahoua Jean Charles kwa mkataba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Stella Club d’Adjame ya nchini humo.

Jean ambaye anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amefunga magoli 12 na kutoa assist tisa katika michezo ya Ligi kuu ya nchini Ivory Coast huku katika Msimu wa 2023/24 akiibuka mchezaji bora wa Ligi kuu ya Nchini Ivory Coast na Klabu yake pia.

Kwa upande wa Klabu ya Yanga wao wamemuongeza mkataba wa miaka miwili Nahodha wake Bakari Nondo Mwamnyeto ambapo anaendelea kusalia kunako klabu hiyo mpaka mwaka 2026.

Mwamnyeto ambaye ni beki wa kati, safari yake ndani ya Klabu ya Yanga ilianza Agosti 2020 aliposajiliwa akitokea Coastal Union ya Jijini Tanga.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement