Paris St-Germain huenda ikalipa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya dunia ili kuipata saini ya winga wa Barcelona na Hispania, Lamine Yamal katika dirisha hili akawe mbadala wa Kylian Mbappe aliyetimkia Real Madrid.

Timu nyingi kubwa barani Ulaya zimevutiwa na kiwango cha kinda huyo mwenye umri wa miaka 16 alichoonyesha katika Ligi Kuu ya La Liga na timu ya taifa ya Hispania, huko Ujerumani kwenye fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro) 2024.


Yamal aliongeza mkataba wake na Barcelona Oktoba mwaka jana, akisaini kubaki Camp Nou hadi 2026. Deco amesema Yamal ataongeza tena mkataba wake 2025 atakapofikisha umri wa miaka 18 na anaamini atabaki klabuni hapo kwa miaka mingi.

Mkataba huo wa Barca unaonyesha kwamba inahitajika Euro 1 bilioni ili kuuvunja mkataba wa Yamal, pesa ambayo inaonekana kuwa ngumu kutolewa na timu yoyote kutokana na sheria za usawa wa matumizi ya pesa zilizowekwa na Uefa.

Hata hivyo, PSG inataka kukaa mezani ili kuzungumza bei na Barca na ikiwa watakubali kushusha kuna uwezekano staa huyo akaonekana mitaa ya Jiji la Paris msimu ujao.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement