Kocha wa Newcastle, Eddie Howe, amekiri Newcastle huenda ikasajili wachezaji kutoka Saudi Arabia mwezi Januari, ili kuboresha kikosi chake kilishosheheni wachezaji majeruhi.

Lakini bosi huyo wa Magpies alisema ni "ajabu" Newcastle ndo inatolewa macho zaidi kwenye usajili baada ya klabu za Ligi Kuu England kupinga kupigwa marufuku usajili wa mkopo kutoka Saudi Arabia itakapofika mwezi Januari. Hiyo inamaanisha Newcastle itakuwa huru kusajili wachezaji kutoka klabu za Saudi Arabia ambayo pia inamilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia.

Newcastle inatazamia kufanya usajili wa kiungo wa zamani wa Wolves, Ruben Neves ambaye amejiunga na Al-Hilal kipindi cha usajili wa kiangazi. Al-Hilal ni moja ya timu inayosimamiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma pamoja na Al-Nassr, Al-Ittihad na Al Ahli, na wanamiliki mastaa kama Cristiano Ronaldo, N'Golo Kante na Riyad Mahrez.

Howe Alisema kuhusu mipango yake Januari: "Newcastle haipo peke yake kuna wapinzani, hii sio juu yetu peke yetu, kila timu ina haki ya kusajili Saudi Arabia, Tunaweza kuruhusiwa kusajili Saudi kama klabu nyingine ulaya, sio kama kuna faida, kila klabu zinastahili pia."

Kutokana na wachezaji wake wengi kuwa majeruhi kocha huyo anataka kulazimisha usajili dirisha dogo kwani kukosekana kwa Sandro Tonali ambaye amefungiwa miezi 10 baada ya kukutwa na hatia ya kucheza kamari, wachezaji kama Sven Botman, Callum Wilson, Harvey Barnes, Dan Burn, Jacob Murphy, Matt Targett na Elliot Anderson wataendelea kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu, ingawa Fabian Schar, Miguel Almiron na Alexander Isak wote walitarajiwa kujumuishwa dhidi ya Chelsea. Lakini Howe akaongeza: "Hatukuwa na mipango ya kusajili Januari Lakini itabidi mabosi waliangalie tena hili kwa sababu tuna wachezaji wengi wapo nje wakiuguza majeraha."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement