Everton inadaiwa kuwa huenda ikalazimika kumuuza beki wao raia wa England, Jarrad Branthwaite katika dirisha hili ili kuepuka adhabu nyingine ya kukatwa pointi kama ilivyokuwa msimu uliopita kwa kukiuka sheria za matumizi ya kifedha.

Timu hii ambayo msimu uliopita ilikatwa pointi zaidi y 10 kwa kukiuka kwao sheria za matumizi ya pesa za Ligi Kuu England itatakiwa kuuza baadhi ya wachezaji ili kuendana na mahesabu.

Inaonekana kwamba itakuwa ngumu kwao kuuza zaidi ya wachezaji wawili kwa wakati mmoja na badala yake inaweza kumuuza Branthwaite pekee ambaye akiondoka timu haitovurugika sana.

Habari ya kuuzwa kwa Branthwaite inaonekana itakuwa nzuri kwa Manchester United ambayo imeanza kuiwania huduma ya fundi huyu kwa muda mrefu.

Jambo linalokwamisha staa huyu kutua Man United inaelezwa ni bei yake lakini kuna uwezekano Everton ikakubali kuipunguza na kumuuza. Mkataba wa staa huyu unamalizika mwaka 2027.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement