Chelsea inatarajia kutuma ofa ya Pauni 60 milioni kwa ajili ya kumsajili winga wa Crystal Palace, Michael Olise, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Chelsea wanataka kumsajili nyota huyo ikiwa ni sehemu wa ramani ya timu yao bila kujali ni kocha gani ataajiriwa.

Chelsea imekuwa ikisajili wachezaji wengi vijana ikiamini watakuwa tegemeo kwa muda mrefu na Olise inamuona kama mmoja wa mastaa wanaofaa katika mpango huo.

Matajiri hao wa London watatakiwa kuzipiku Manchester United na Man City ambazo zinahusishwa na huduma yake kwa muda.

Staa huyu wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake unamalizika mwaka 2027 na msimu huu amecheza mechi 19 za Ligi Kuu England na kufunga mabao 10.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement