Mabosi wa Chelsea wapo tayari kumtoa straika wao na Ubelgiji, Romelu Lukaku, 31, na kiungo raia wa Italia, Cesare Casadei, 21, kwenda Napoli kama ofa kwa ajili ya kuipata saini ya straika wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen, 25, ambaye timu yake inahitaji Pauni 110 milioni ili kumuuza.



Chelsea ambayo kwa sasa inachunguzwa juu ya masuala ya kukiuka sheria za matumizi ya pesa haitaki kutoa kiasi hicho chote kwa sababu kitazidi kuwaweka katika hali mbaya ya kukumbana na adhabu kutoka kwa mamlaka za soka.

Hivi karibuni timu nyingi zilidaiwa kujiondoa katika mchakato wa kumsajili Osimhen kutokana na bei yake na Chelsea imeamua kujiongeza kwa kutaka kuwatoa baadhi ya wachezaji ili itoe pesa kiduchu.

Mpango wa kumjumuisha Lukaku katika dili hili unaonekana huenda ukachochea Napoli kukubali kwani kocha Antonio Conte anadaiwa kuwasilisha jina la straika huyo hapo awali akitaka asajiliwe kama mbadala wa Osimhen. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

Lukaku hakuwa na bahati huko Euro mabao yake yakikataliwa.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement