Chelsea bado ina mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Nico Williams ambaye anawindwa na Arsenal ambayo inadaiwa kumpa ofa kubwa itakayoenda kumfanya kuwa mchezaji namba mbili kwa kulipwa zaidi katika kikosi cha washika mitutu hao.

Williams ambaye amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Hispania kwenye michuano ya Euro inayoendelea huko Ujerumani, mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa staa huyu na aliwaambia mabosi wake kwamba wafanye kila linalowezekana ili kiungo huyo atue.

Bilbao ipo tayari kumwachia ikiwa timu inayomhitaji itatoa ada ya kuvunja mkataba wake inayodaiwa kuwa ni Euro 55 milioni ambayo inaweza kulipwa na timu hizi mbili.

Katika msimu uliopita, alicheza mechi 39 za michuano yote, akafunga mabao nane na kutoa asisti 19.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement