Klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani inavutiwa na kiungo wa klabu ya Sunderland, Jobe Bellingham ndugu wa kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham.

Jobe (18) raia wa England ambaye ameichezea Sunderland mechi 45 kwenye Ligi ya Championship tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka Birmingham msimu uliopita ameifungia Sunderland magoli 7.


Dortmund inataka kuipata saini ya Jobe msimu mmoja baada ya kumfanya kaka yake (Jude) kuwa mmoja wa wachezaji bora wa soka Duniani kwa sasa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement