Barcelona imemuweka katika rada zake kiungo wa Arsenal na Ghana, Thomas Partey, 30, na inataka kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Partey anadaiwa kuwa mmoja kati ya mastaa ambao Arsenal inataka kuwauza na kutumia pesa itakazopata kufanya usajili wa wengine mwisho wa msimu huu.

Barcelona inataka kumsajili Partey ambaye anasumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara kwa sababu wanaona watampata kwa bei rahisi na pia watamtumia wanavyotaka. Kwa sasa Barcelona imekuwa ikipambana kusajili kiungo wa chini na mara kadhaa ilihusishwa na Bruno Guimaraes wa Newcastle Unitred, lakini changamoto kubwa inaonekana kuwa ni bei yake.

Partey amekuwa hapati muda mwingi wa kucheza ndani ya Arsenal kutokana na majeraha hayo na msimu huu amecheza mechi 13 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025.
You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement