Daniel Amoah aliyedumu kwa miaka minane ndani ya Azam FC amepewa mkono wa kwaheri, hivyo hatakuwa mmoja wa wanajeshi watakaopambania timu hiyo kwa msimu ujao wa 2024/25.

Beki huyo wa kati alijiunga na Azam, mwaka 2017 akitokea Medeama FC ya Ghana.

Azam ilimuona kitasa huyo alipokuja na Medeama kucheza dhidi ya Yanga katika mechi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika Julai 16, 2016 mchezo huo uliisha kwa sare ya bao 1-1.

Baada ya kumaliza msimu wa 2022/2023 Amoah aliongeza mkataba wa miaka miwili uliokuwa uishe mwaka 2025, taarifa zinadai nyota huyo ataendelea kuonekana katika Ligi Kuu Bara baada ya Simba kuonyesha nia ya kumhitaji.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement