Arsenal inamtazama mlinda lango wa zamani na mchezaji wa kimataifa wa Poland Wojciech Szczesny, 34, pamoja na mlinda lango wa Brighton Muingereza Jason Steele na kipa wa Ajax Mjerumani Diant Ramaj wakitafuta atakayeziba nafasi ya Mwingereza Aaron Ramsdale, 25, ambaye anatarajiwa kuondoka The Gunners.

Arsenal pia wanafikiria kumnunua kipa wa Everton na England Jordan Pickford, 30 katika dirisha la usajili la majira ya joto.

The Gunners wanalenga kusajili beki, kiungo na mshambuliaji huku wakipania kuimarisha kikosi cha meneja Mikel Arteta.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement