KLABU YA AL ITTIHAD YA SAUDI ARABIA YAANZA MAZUNGUMZO YA KUIPATA SAINI YA KIPA WA CHELSEA KEPA ARRIZABALAGA
Kipa wa Chelsea, Mhispania Kepa Arrizabalaga, 29, yupo katika mazungumzo na mabosi wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia inayohitaji kumsajli katika dirisha hili baada kuibuka kwa ripoti kwamba hatma yake katika kikosi cha Chelsea haijajulikana hadi sasa.
Kepa ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Real Madrid, ameliambia benchi la ufundi la Chelsea anataka kuhakikishiwa nafasi ya kucheza ikiwa atarudi.
Arrizabalaga alijiunga na Madris katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana akienda kuchukua nafasi ya Thibaut Courtois ambaye alipata majeraha wakati wa maandalizi ya msimu.
Mwanzoni Kepa alikuwa namba moja na ikaelezwa kwamba angeweza kusaini mkataba wa kudumu, lakini kati kati ya msimu alipoteza namba mbele ya Andriy Lunin.
Hakuna uhakika ikiwa yupo tayari kutimkia Saudia na kuacha kucheza soka la kiushindani barani Ulaya ingawa ofa iliyowekwa inaripotiwa kufikia mara nne ya mshahara wake wa sasa wa Pauni 150,000 kwa wiki.