Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa kiungo, Luis Miquissone hatakuwa sehemu ya kikosi chake kwa msimu ujao baada ya mkataba wa nyota huyo raia wa Msumbiji kufikia ukomo.

Wekundu wa Msimbazi wamefikia uamuzi huo kufuatia kiwango kisichoridhisha cha nyota huyo wa zamani wa Al Ahly.

Miquissone anaondoka Simba Sc kwa mara ya pili baada ya kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi mara mbili kwa nyakati tofauti.

Miquissone alijiunga na Mnyama mnamo Januari 2, 2020 akitokea Mamelodi Sundowns kabla ya kutimkia Al Ahly Agosti 21, 2021.

Mnamo Julai 22, 2023 Miquissone alirejea tana Msimbazi kwa uhamisho huru kutokea Al Ahly kabla ya kuondoka tena kama mchezaji huru baada ya kutamatika kwa mkataba wake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement