Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes amesema kitu kuhusu kipa veterani Tom Heaton ambaye yupo kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga huko Old Trafford.

Kipa Heaton, 38, amekuwa kwenye kikosi cha Man United tangu aliporudi Old Trafford mwaka 2021. Alijiunga akitokea Aston Villa kwenda kuongeza nguvu kwenye idara ya makipa ya kikosi hicho.

Heaton angeweza kuondoka kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake kumalizika, lakini Man United ipo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kumsainisha dili jipya.

Wakati huo, Heaton anajiandaa kujiunga na kikosi cha England kilichopo kwenye fainali za Euro 2024 huko Ujerumani. Hatacheza mechi yoyote, lakini atashiriki kwenye mazoezi ya kikosi hicho cha Three Lions.

Mwenyewe aliandika kwenye Instagram: “Ni heshima kubwa kuitwa kujiunga kwenye kikosi cha Gareth. Kuitwa kwenye michuano mikubwa, kwenda kusaidia ni kitu kinachonipa uzoefu wa kutosha. Tuna kikosi kizuri, nasubiri kwa hamu kwenda kujiunga nao.”

Na sasa kiungo Fernandes, ambaye ni mchezaji mwenzake huko Man United alisema kitu kuhusu kipa huyo: “Kiwango bora siku zote kinapata nafasi popote pale. Hongera kwako kaka mkubwa.”

Hata hivyo, Fernandes si mchezaji pekee wa Man United alimtumia Heaton meseji ya pongezi, huku wakali wengine waliofanya hivyo ni beki Diogo Dalot na kipa Altay Bayindir pamoja na kocha Benni McCarthy naye aliweka neno lake.

Akimzungumzia Heaton, kocha wa England, Gareth Southgate alisema: “Nimefurahishwa na Tom kukubali kujiunga nasi Ujerumani. Uzoefu wake unahitajika sana kwenye idara yetu ya makipa inayoongozwa na Martyn Margetson.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement