Jordan Henderson Awekewa Dau Nono Saudi Arabia
Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson anafikiria kuondoka katika klabu hiyo na kwenda kwenye klabu ya Al-Ettifaq inayofundishwa na Steven Gerrard ya nchini Saudi Arabia. Bado hawajawasilisha ofa rasmi kwa kiungo huyo wa kati wa England (33) lakini matamanio ya kupata huduma ya mchezaji huyo ni makubwa sana.
Mkataba wa Jordan Henderson ndani ya klabu ya Al Ettifaq utakua na mchanganuo huu kama atakubali kujiunga na klabu hiyo.
Mwaka - £36,400,000
Mwezi - £3,033,333
Wiki - £700,000
Siku - £99,726