Mshambuliaji wa TP Mazembe, Jean Othos Baleke ambaye alikuwa kwa mkopo kunako klabu ya Al Ittihad ya Libya amethibitisha kujiunga na Young Africans Sc kama mchezaji mpya klabuni hapo kwa msimu ujao wa 2024/25.

Kupitia Insta Story yake Baleke ameposti picha akiwa ndani ya uzi wa Yanga Sc ikiwa ni Taarifa ya moja ya chombo cha habari kilichothibitisha ujio wake Jangwani. 

Nyota huyo anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na klabu hiyo baada ya kusitisha mkataba wake wa mkopo na miamba hiyo ya Libya na kujiunga na Wananchi. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement