Inaelezwa kiungo wa Bayern Munich, Jamal Musiala amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya aliyowekewa mezani na mabosi wa Bayern akidaiwa kutaka kuondoka mwisho wa msimu huu ambapo Manchester City na Liverpool zinadaiwa kumhitaji.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Star, Manchester City na Liverpool, zote zimekuwa zikituma maskauti kwenda Ujerumani kwa ajili ya kumtazama staa huyu na hivi karibuni walikuwepo kwenye mchezo dhidi ya Bayer Leverkusen

Inaelezwa Bayern imeweka mezani ofa ya Pauni 150,000 kwa wiki lakini staa huyu amewaambia kwamba hatosaini kwa sababu anafikiria kuondoka mwisho wa msimu. Man City na Liverpool zinaripotiwa kuwa sehemu ya staa huyo kukataa ofa hiyo na Man City ndio inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumsajili staa huyu alicheza mechi 25 akiwa na Bayern msimu huu.

Chelsea pia ni moja ya timu zinazodaiwa kumhitaji na huenda ikaingia kwenye vita kwenye wiki chache zijazo. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement