IMESIBITISHWA NA NYOTA SAMATTA KWENDA UFARANSA KUJIUNGA NA CLUB HAVRE ATHETIC
Mbwana Ally Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ambaye pia amecheza klabu kama Genk, Aston Villa, Fenerbahçe, na PAOK, ameidhinisha rasmi kusajiliwa na Le Havre, kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram samatta amethibitisha taarifa hiyo,Akisema ;
"Kwa furaha kubwa, ninatangaza kujiunga na @hac_foot!! Katika wiki chache zilizopita nimejifunza mengi kuhusu klabu hii ya kihistoria na maalum, na naamini katika mradi unaoendelea kujengwa. Asante sana kwa klabu kwa kuniamini, na ninatarajia kutoa asilimia 100 katika @Ligue1. Siwezi kusubiri kuanza – allez les ciel et marine!"
Kwa maneno yake hayo Nyota huyu ameidhinisha rasmi kusajiliwa na Le Havre Athletic Club (HAC) tarehe 5 Agosti 2025 ,Pia amejiunga kwa mkataba wa misimu miwili mpaka Juni 2027, akichukua jezi namba 70, na kuwa Mwanza wa kwanza wa Kitanzania kujiunga rasmi na HAC.
Ikumbukwe Samatta alifika HAC akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na PAOK Saloniki, ambapo msimu uliopita alifunga mabao 5 katika mechi 20, na kutoa pasi za mabao 3 huku HAC imekuwa ikihitaji mbadala wa mashambuliaji waliokwenda, kama André Ayew na Ahmed Hassan, na ilimwalika Samatta kwa uzoefu wake mkubwa kama kiungo wa kuimarisha safu ya mbele ya timu hiyo.



