Klabu ya Azam imemrejesha nyota wa zamani wa timu hiyo Himid Mao ambaye amesainimkataba wa mwaka mmoja hadi 2026.Mao aliondoka azam FC mwaka 2018, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 10 tangu mwaka 2008.


Himid Mao anacheza kama kiungo mkabaji, nafasi muhimu inayohitaji nidhamu, busara ya mchezo, na uwezo wa kusambaza mipira kwa ufanisi. Ana uwezo mkubwa wa kukatiza mashambulizi ya wapinzani kabla hayajafika kwa safu ya ulinzi.


Anaeleweka kama mchezaji mwenye maono ya kiufundi, anayejua lini apunguze kasi ya mchezo, au afanye pressing. Uelewa wake mkubwa wa mchezo humfanya awe msaada mkubwa kwa mabeki na viungo washambuliaji.

Amevalishwa unahodha kwenye timu ya Azam FC na pia mara kadhaa ameiongoza Taifa Stars. Ana sifa ya kuwa kiongozi mwenye nidhamu, mhamasishaji na mchezaji anayeheshimika vyema uwanjani na nje ya uwanja.

Mbali na Himid hadi sasa Azam imesajili nyota wanne wapya ambao ni pamoja na Lameck Lawi, Muhsin Malima na Aishi Manula.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement