Klabu ya Yanga imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Joseph Guédé Gnadou akiwa mchezaji huru baada ya kuachana klabu ya Tuzlaspor ya Uturuki.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tatu za mbele ikiwemo mshambuliaji wa kati na wing azote mbili anatumia mguu wa kulia. Usajili huo unaenda kuimarisha eneo la ushambuliaji la Yanga ikiwa ni matakwa ya kocha Miguel Gamondi baada ya kutokuwa na straika wa uhakika baada ya kutorishwa na kiwango cha waliokuwepo.

Gnadou ametua kuziba nafasi ya Hafiz Konikoni ambaye ametolewa kwa mkopo katika klabu ya Dogan Birlig ya Uturuki kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. Awali Yanga ilikuwa imsajili mshambuliaji Ismail Auro Agoro raia wa Togo lakini kocha wao Miguel Gamondi akamkataa kufuatia staa huyo wa FAR Rabat kupoteza nafasi kwenye kikosi chake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement