Shirikisho la Soka la Morocco limempa kandarasi kocha raia wa Hispania Jorge Vilda kufundisha timu ya taifa ya kandanda ya wanawake.

Jorge Vilda anarithi mikoba ya Reynald Pedros ambaye aliisaidia Morocco kufuzu kwa Kombe lao la kwanza la Dunia la Wanawake mnamo 2023 na kuwaongoza hadi hatua ya 16 bora, ambapo walitolewa na Ufaransa.

Shirikisho la Soka la Morocco linamshukuru Pedros kwa kazi aliyoifanya zaidi kuisaidia timu kufuzu kwa raundi ya pili ya Kombe la Dunia".

Vilda aliiongoza Uhispania kutwaa taji la Kombe la Dunia la Wanawake majira ya joto, walipoilaza England 1-0 kwenye fainali.

Uhispania iliishinda Uingereza katika fainali ya Kombe la Dunia mnamo Agosti 20 lakini ushindi huo ulifunikwa na Rubiales kumbusu fowadi Jenni Hermoso, jambo ambalo amesema halikuwa la maafikiano.

Jorge Vilda alifukuzwa kazi ndani ya mwezi mmoja huku kukiwa na matokeo mabaya ya kashfa ya Luis Rubiales.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement