Simba kuinasa saini yaaliyekuwa nyota wa Tanzania Prisons, Edwin Balua kwa mkataba wa miaka mitatu, winga huyo amedai hahofii ushindani uliopo ndani ya kikosi hicho kwani amejipanga kwa ajili ya kuonyesha makali yake.

Balua alisema kusajiliwa kwake ndani ya timu hiyo ni isharatosha kwamba ana uwezo wa kukichezea kikosi hicho hivyo ni nafasi ya kuonyesha ushindani kwa lengo lakufikia malengo ya klabu.

"Simba ni timu kubwa ambayo kila mchezaji ana ndoto za kuichezea naniseme wazi malengo yangu yametimia kupata nafasi hii muhimu maishani mwangu, nina kazi kubwa ya kufanya ila nawaahidi viongozi na mashabiki sitowaangusha kwao," alisema.

Balua aliyekamilisha idadi ya wachezaji sita waliosajiliwa na timu hiyo katika dirisha hili dogo la usajili lililofungwa Januari 16 mwaka huu, aliongeza deni alilonalo ni kubwa ingawa anaomba zaidi apewe muda kwani miguu yake itaongea zaidi.

"Naamini katika subra kwa sababu timu niliyotoka na huku ni tofauti na haziwezi kulingana, mimi ni mchezaji nisiye amini kushindwa hivyo nitashirikiana na wachezaji wenzangu na kila nitakapopata nafasi nitaonyesha kwanini nimesajiliwa hapa." Kocha na mchezaji wa zamani Simba, AbdallahKing' Kibadeni alisema licha tu ya presha kubwa inayomkabili ila anaamnini ana uwezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement