Beki wa zamani wa Yanga anayedaiwa kusajiliwa Azam FC, Djuma Shabani, ni kama ameanza kujishtukia mapema baada ya kusema licha ya kuwa nje kwa karibu nusu msimu, lakini amebaini msimu huu kuna ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara.

Djuma aliyecheza kwa mafanikio ndani ya Yanga akitwaa nao mataji mawili ya Ligi, ASFC na Ngao ya Jamii, 

Ligi Kuu inaendelea kukua msimu hadi msimu, hivyo anaamini atakuwa na kazi ngumu atakapokamilisha mambo yake dirisha dogo.

"Hakuna mchezaji mpenda mafanikio ambaye hatamani kucheza Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni bado sina timu ila dirisha dogo kila kitu kitakuwa wazi ni wapi nitacheza. Kuhusu ushindani kwa sasa ni mkubwa hii ni

kutokana na kukua kwa ushindani kwa timu jambo ambalo limekuwa chachu ya wachezaji wengi kutamani kuendelea kucheza soka la Tanzania,)" alisema beki huyo wa zamani wa AS Vita ya DR Congo.

Djuma alisema endapo mambo yake yataenda sawa kama walivyopanga anaamini atakuwa na wakati mgumu wa kuipambania timu yake kufikia malengo licha ya kuiona inafanya vizuri akiwa yupo kambi ya Azam tangu alipotemwa na Yanga.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement