DAU LA LIVERPOOL LA KUMNASA MBAPPE NI KUBWA KULIKO MADRID
Kylian Mbappe Staa huyo wa Paris Saint-Germain ambaye yupo katika miezi sita ya kumalizia mkataba wake anatarajiwa kujiunga na Real Madrid akiwa mchezaji huru.
Inadaiwa Mbappe ambaye anaruhusiwa kuzungumza na klabu yoyote kwa sasa kuhusu usajili wake, amekubaliana na Madrid kuhusu maslahi yake na mambo mengine kadhaa licha ya kuwa Liverpool nayo ni moja ya Klabu inayoonesha nia ya kutaka kumsajili.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa dau la mshahara ambalo Liverpool wametenga kumpatia ni kubwa kuliko kiwango kilichotengwa na Madrid lakini Mbappe anaweza kwenda Hispania kutokana na historia ya mafanikio ya Madrid katika kutwaa mataji.