COPCO FC YAONGEZA NGUVU KUEPUKA KUSHUKA LIGI YA NBC CHAMPIONSHIP
Copco FC ya Mwanza yaongeza nguvu kuepuka kushuka Ligi ya Championship baada ya kuamua kuwachukua washambuliaji wakongwe Dany Mrwanda, Salum Ngadu na Morice Mahela kwenye dirisha dogo lililofungwa Januari 15, mwaka huu ilikutibu tatizo la upachikaji wa mabao linaloitesa.
Mrwanda amejiunga na timu hiyokutoka Ken Gold alikokuwa meneja, Morice Mahela ametokea Tabora United na Salum Ngadu akiwa mchezaji huru,lakini nyota hao hawajaanza kucheza na wanatarajia kuanza kukiwasha katika mchezo ujao dhidi ya Stand United.
Timu hiyo inashika nafasi ya 15 ikiwa katika msimamo ikiwa na pointi 13 baada ya kuambulia sare nne, ushindi mara tatu na kupoteza michezo 11, huku ikifunga mabao 16 na kuruhusu 27.
Nyota hao wanatarajiwa kuongeza uhai katika eneo la ushambuliaji lililokuwa linaongozwa na Abdulkarim Segeja aliyejiunga na Tanzania Prisons akiwa amefunga mabao manane msimu huu. Akiwazungumzia wachezaji hao, Kocha wa Copco FC ambayo ni msimu wake wapili Championship, Feisal Hau amesema anaamini ujio wao una kwenda kuongeza kitu na kutibu tatizo laufungaji katika kikosi kwani amechanganya damu changa na wazoefu.
Amesema amepata matumaini ya kikosikuwa bora baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara United mwishoni mwawiki iliyopita, hivyo hawezi kukatatamaa kwani atafanya vizuri na kikosi ilikuhakikisha hawashuki daraja mwishoni mwa msimu.
"Tatizo letu kubwa kuanzia raundi yakwanza lilikuwa ni kumalizia na kipa.Tumetibu eneo la kipa na hata mbelekuna usajili tuliufanya. Tunaye Salum Ngadu tumemleta lakini ndani ya sikumbili hizi kapata homa, tuna Danny Mrwanda mchezaji mzoefu," amesema
"Ana matatizo kidogo (Mrwanda) nafikiri kuanzia mechi ya Stand (Ijumaa) wote unaweza kuwaona uwanjani. Naamini watatusaidia mbele katika eneo la ufungaji wa mabao. Nyinyi wenyewe mmeona kuna watu wametoka, lakini kuna wengine wameingia."
"Sisi kwenye selection (uchaguzi) ya wachezaji huwa tunajitahidi nafikiri mmeona kuna vijana wadogo damu changa, lakini wana uwezo wakupambana kushirikiana na wakongwekama Mrwanda na Ngadu naamini matokeo (mazuri) yatapatikana."